TUME
YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR INATANGAZA NAFASI YA KAZI YA MSIMAMIZI WA
UCHAGUZI NA MSAIDIZI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO KWA MAJIMBO YOTE YA
UCHAGUZI YA ZANZIBAR.
MUOMBAJI WA NAFASI YA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI NA MSIMAMIZI MSAIDIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO ANATAKIWA AWE NA SIFA ZIFUATAZO:-
- AWE MZANZIBARI,
- AWE NA UMRI USIOPUNGUA MIAKA 35
- AWE NA ELIMU ISIYOPUNGUA DIPLOMA AU UZOEFU KATIKA UONGOZI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA UCHAGUZI ZA JIMBO USIOPUNGUA CHAGUZI TATU.
- UZOEFU WA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
- AWE NA UWEZO WA KUTEKELEZA DHAMANA ZAKE BILA YA USIMAMIZI,
- AWE NA UWEZO WA KUIFAHAM JAMII ILIYOMZUNGUKA,
- UWEZO WA KUTEKELEZA SHERIA ZA UCHAGUZI,
- AWE NA UWEZO WA KUTUNZA KUMBUKUMBU NA KUFANYA HESABU KWA USAHIHI,
- AWE NA UWEZO WA KUANDIKA RIPOTI
- ASIWE NA USHABIKI WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA, NA
WAOMBAJI
WA NAFASI HIZO WATATAKIWA KUOMBA KWA MAANDISHI KWA MKURUGENZI WA
UCHAGUZI, TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR. KATIKA MAOMBI HAYO WAAMBATANISHE
CV, NAKALA ZA VYETI VYA KUMALIZIA MASOMO NA KITAMBULISHO CHA MZANZIBARI
MKAAZI.
KILA
MWOMBAJI WA NAFASI ZILIZOTAJWA, ANATAKIWA AHAKIKISHE KUWA ANAOMBA
KUFANYA KAZI KATIKA JIMBO AMBALO YEYE NI MPIGA KURA ILI AWEZE KUTUMIA
HAKI YAKE YAKISHERIA YA KUPIGA KURA.
BARUA ZA MAOMBI ZITUMWE KWA ANUANI IFUATAYO:-
MKURUGENZI WA UCHAGUZI,
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
P.O.BOX 1001
ZANZIBAR.
KWA
WAOMBAJI WA UNGUJA BARUA ZA MAOMBI ZIWASILISHWE OFISI KUU YA TUME YA
UCHAGUZI YA ZANZIBAR, ILIYOPO MAISARA NA WAOMBAJI WA PEMBA MAOMBI YAO
YAWASILISHWE OFISI NDOGO YA TUME YA UCHAGUZI ILIYOPO CHAKECHAKE – PEMBA.
SIKU YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 08 /2/2016 MUDA NA SAA ZA KAZI.
PIGA KURA KWA AMANI UPATE MAENDELEO NCHINI
TANGAZO HILI LIMELETWA KWENU NA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment